E-sir · Lyrics

Hamnitishi

by E-Sir ft Talia

[Intro]

Vitisho vya peni mbili

Vitanifanya mimi nini?

 

[Chorus-Talia]  (x 2)

Hamnitshi tishi,

Hamnibabaishi,

Maisha n’nayoishi

Hayanikubali.

 

[E-Sir]

Bila spare tyre, ‘nasafiri kwenye barabara

ya maisha bila kutaka

Saa yoyote ‘naweza pata puncture

Kwa hivyo naendesha gari yangu polepole sana

Allahu Akbar!

Mungu ni mkubwa.

Asante Baba kwa kunisaidia kujua

Ukiotesha mazuri, mazuri utavuna

Tangu siku yangu ya kuzaliwa

mpaka siku hii tumefika

Hakuna mtu angewahi fikiria sifa za E-Sir,

Yule kijana aliyekuwa akikaa jobless corner

Akisaka bomba ijapokuwa amesoma,

Angekuwa akisikizwa kwa radio

Matamshi kukubaliwa na kila masikio

Kuchezewa kuku dance au chakacha

ndiyo matokeo.

Leo ni leo, nikiregea cha kwangu nitapepea

si mimi

ni maisha ninayoishi

Hamnitishi, Hamnibabaishi.

 

[Talia]

Hamnitishi tishi

[Chorus] (x2)

 

Niliambiwa kidole kimoja hakiwezi kuua chawa

Ndege hawezi kupaa bila mabawa

Basi bila nyinyi singefika hapa

Bila mpira utacheza aje game-u ya kananda

Asanteni, kwa kunipa moto wa kuandika

Asanteni wakati wa vita, kunisimamia

Asanteni, kwa kuwika

Mtu akimshika, ametushika

Na hiyo ni shida

Pirates, mpaka kufa

Na singependa  kukufa bila nyinyi kujua

Mimi si mimi bila nyinyi

Na nyinyi ndiyo maisha ninayoishi

Nd’o sababu hawanitishi.

 

[Talia] (x2)

Hamnitishi, Hamnibabaishi

Maisha n’nayoishi

Hayan’kubali mimi!

 

[E-Sir]

Nimefika, ongeza volume na ukaribie speaker yatatumia

kila mtu aliyenisaidia, kutoka Ogopa DJs

mpaka InDaBooth DJs walio-call presenter

na kumwambia ‘Replay! Hiyo ngoma imetubamba, asanta.’

Ndiyo sababu polisi, ma-MC, maadui, hii industry

Hawanitishi, hawanibabaishi

Maishi ninayoishi, hayanikubali.

 

[Chorus] (x4)

Hamnitishi tishi (x4)

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s